DIMPOZ ADAI KUCHANGIA NYIMBO YA DIAMOND

Share it:

img_52469714273651

Msanii wa muziki nchini, Ommy Dimpoz amefunguka na kudai kuwa mistari illiyokuwepo kwenye nyimbo ya msanii Diamond ya ‘Nasema nawe’ na yeye alichangia kuandika kipindi bado ni marafiki. Msanii huyo alifunguka na kuamua kuweka mambo wazi kutokana na tofauti zilizokuwepo baina yake na Diamond. “Mimi nataka kusema kitu kimoja, sijawahi kusema sehemu yoyote hapa, mfano kwenye nyimbo ya mduara ya D Nasema Nawe, mimi nimechangia kwa asilimia kubwa uandishi wa ile nyimbo. Sio kwamba D hajui kuandika, anaandika vizuri na nawaheshimu ni moja ya waandishi bora kabisa,” amesema Ommy. Staa huyo ametolea mfano mstari aliochangia ni wa verse ya pili usemao ‘zingifuli zingifuli usozinga mahala ukakaa.’ Muimbaji huyo amesema hata kwenye verse ya kwanza kuna maneno ameyaandika lakini hakuwahi kutaka apewe credit. “Sikufanya vile kwasababu nilipwe au nipewe credit. Lakini nataka tu niseme kuwa mashabiki kuna vitu vingine vingi hawajui,” amesema Ommy. Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake kipya kabisa alichomshirikisha msanii mwenzake Alikiba.
Share it:

ENTERTAINMENT

Post A Comment: