TUME YA MUFTI YAIBUA MAZITO

Share it:
bakw

Hatimaye Tume iliyoundwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir kufuatilia mali za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) imekabidhi ripoti ya awali kwa mufti huyo huku ikiainisha baadhi ya mali za Waislamu zilizoporwa kwa hila. Tume Ya Mufti Yaibua Mazito Bakwata ­ Tanzania ­Mwenyekiti wa Tume hiyo, Sheikh Abubakar Khalid amesema tume hiyo imefanya kazi kubwa hadi kukamilisha ripoti hiyo ya kwanza licha ya kutokuweka wazi mali walizobaini kuporwa na kueleza kuwa jambo hilo litafanywa na Mufti mwenyewe kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za ripoti hiyo. Sheikh Khalid amesema tume hiyo ilipewa miezi mitatu, lakini kazi hiyo imekuwa ni ngumu hasa kwa kuzingatia kuwa baraza hilo lina mali nyingi nchini kote na shughuli za tume hiyo ilikuwa ni kuhoji wahusika kwa mikataba waliyoingia. “Ilikuwa ni ngumu kuwapata kwa nafasi zao , tumefanikiwa kukamilisha ripoti ya kwanza kwa baadhi ya mali tu na mikataba ya mkoa wa Dar es Salaam, shughuli nyingine zitaendelea baadaye. Ripoti hii ni nusu ya ripoti ya awali ya kazi ya Dar es Salaam na wataendelea katika mikoa yote hadi watakapokamilisha na ndio sababu ya kuomba waongezewe muda na wanamshukuru Mufti kwa kuwakubalia jambo hilo kwa kuwaongeza miezi mitatu mingine,” amesema Sheikh Khalid. Amesema kuwa walipewa hadidu za rejea zilizokuwa zikiwaeleza kufuatilia viwanja, majengo pamoja na mali nyingine zilizokuwa zikimilikiwa na Waislamu na ndilo walilolitekeleza. Naye Mjumbe wa tume hiyo, Shehe Hamis Mataka amesema tume hiyo haina mamlaka ya kueleza kilichomo ndani ya ripoti hiyo, bali mufti ndio mwenye mamlaka ya kueleza yaliyomo na kuyafanyia kazi. “Mufti alitoa hadidu za rejea saba ambazo ni kufuatilia mali za baraza hilo, kuangalia hesabu za baraza, kuangalia namna ya kuboresha mifumo pamoja na mengine,” amefafanua. “Haya yote ndiyo yanayoshughulikiwa na tume, lakini kwa kuanzia kutokana na ukubwa wa jambo, tume imeshughulikia yale yanayohusu Dar es Salaam, sasa ukiulizia Dar es Salaam Bakwata ina viwanja vingapi? Ina viwanja kadhaa, lakini kimojawapo ni Chang’ombe na mgogoro huo unajulikana,” amesema Mataka.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: