WAWILI KUZABA NAFASI YA LUKAKU

Share it:
Meneja wa klabu ya Everton, Ronald Koeman ameanza maandalizi ya kuziba nafasi itakayoachwa wazi na mshambuliaji wake kutoka nchini Ubelgiji, Romelu Menama Lukaku ambaye huenda mwishoni mwa msimu huu akaondoka Goodison Park.
Koeman, amedhamiria kutenga kiasi cha Pauni milioni 50 kwa ajili ya usajili wa wachezaji Cedric Bakambu na Willian José da Silva ambao kwa pamoja wanacheza katika ligi ya nchini Hispania.
Koeman ameanza mikakati hiyo kwa kuamini endapo atafanikisha usajili wa wachezaji hao wawili mwishoni mwa msimu huu, atakua amefanikisha kuziba nafasi ya Lukaku, ambaye juma lililopita aliweka wazi mpango wake wa kutosaini mkataba mpya na uongozi wa Everton.

Image result for Cedric Bakambu and Willian José da Silva

Bakambu ambaye ni mzaliwa wa nchini Ufaransa mwenye asili ya Jamuhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo, amekua na msimu mzuri katika ligi ya nchini Hispania akiwa na klabu yake ya Villareal.
Mshambuliaji huyu ana umri wa miaka 25, alisajiliwa na Villareal mwaka 2015 akitokea Bursaspor ya nchini Uturuki, na tayari ameshaitumikia Nyambizi Ya Manjano katika michezo 45 na kufunga mabao 15.

Image result for Willian José da Silva
Kwa upande wa Jose mwenye umri wa miaka 25, amewahi kucheza kwa mkopo katika kikosi cha Real Madrid mwaka 2014, na amekua na umuhimu mkubwa akiwa na klabu yake ya Real Sociedad msimu huu.
Mshambuliaji huyu raia wa nchini Brazil, tayari ameshafunga mabao 11 katika ligi ya Hispania msimu huu, na anafuatiliwa na wasaka vipaji wa baadhi ya klabu za barani Ulaya.


Wachezaji hawa wawili thamani yao ni Pauni milioni 25 kwa kila mmoja, hivyo endapo Everton watafanikisha mpango wa kusawajili watalazimika kutumia Pauni milioni 50.
Share it:

SPORTS

Post A Comment: