Wafanyabiashara 13 kutoka Wilaya za Babati na Hanang’ Mkoani Manyara, wamesalimisha katoni 1,540 za pombe aina ya viroba zenye thamani ya sh. 140 milioni.
Wafanyabiashara hao wamesalimisha katoni hizo za pombe aina ya viroba kabla ya upekuzi ulioendeshwa na polisi, Maofisa wa Usalama wa Taifa, chakula na dawa (TFDA) na mamlaka ya mapato nchini (TRA).
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Francis Massawe, amesema kuwa wafanyabiashara hao wamesalimisha wenyewe viroba hivyo bila kushurutishwa.
Hata hivyo, Kamanda Massawe amesema katika wilaya ya Hanang’ zimesalimishwa katoni 871 na kwa wilaya ya Babati zilisalimishwa katoni 669 na wafanyabiashara hao wanaopaswa kupongezwa kwa hatua hiyo
Post A Comment: