Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wakuu wa magereza nchini ambao watashindwa kutimiza dhana ya uzalishaji mali ambayo ni agizo la Rais John Magufuli.
Aidha, Jeshi la Magereza Tanzania limetaja changamoto tano kuu ambazo zinakabili jeshi hilo hali ambayo inakwamisha ufanisi katika mipango yao.
Masuani alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wakuu wa vituo vya magereza Tanzania Bara unaofanyika katika Bwalo la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri alisema iwapo wakuu wa magereza watatumia wafungwa waliopo uzalishaji utaongezeka hivyo kuondokana na tabia ya kulalamika ufinyu wa bajeti.
Alisema pamoja na vigezo mbalimbali vya kupima wakuu wa magereza kigezo kingine kitakuwa ni kuangalia kasi ya uzalishaji kwa eneo husika.
Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.
“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.
Naibu waziri alisema anaamini kupitia jeshi hilo ajiraz itaongezeka, uchumi utakuwa na maendeleo ya nchi yatapatikana kwa haraka hivyo lengo la 2025 kukamilika.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali Magereza, Dk. Juma Malewa alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ufinyu wabajeti, madeni ya watumishi, makaziduni, ukosefu wa posho na vitendea kazi kama usafiri.
Alisema katika kutatua changamoto ya usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.
Dk. Malelwa alisema pia wameanza kutatua changamoto ya makazi ambapo Rais Magufuli ametoa sh. bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 320 katikakambiyaUkonga.
Kamishna Jenerali Malelwa alisema hadi sasa wamepokea sh. bilioni 5 ambazo zimeanza kutumika kujenga nyumba hizo 320 zinazojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA).
Alisema wao wamejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inapatikana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivyo utatuzi wa changamoto hizo utakuwa suluhu sahihi kwao.
“Tumedhamiria kuongeza uzalishaji na kufufua viwanda mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini tunaomba changamoto nilizo zitaja zitatuliwe kwa wakati,” alisema.
Akizungumzia dhana hiyo ya viwanda Mkurugenzi waViwanda, Naibu Kamishna wa Magereza Edith Mallya alisema utekelezaji wa agizo la Serikali umeanza katika baadhi ya viwanda kama MbigiriMorogoro na Karanga.
Post A Comment: