Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya
Tatu, Frederick Sumaye ameiomba Serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika
kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Ameyasema hayo Jijini Dar es
Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa kama Serikali
itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa
litafikia malengo yake liliyojiwekea ya kupunguza hali ya umasikini na kuongeza
pato la taifa kwa ujumla.
“Taifa letu litasonga mbele kama
Serikali itakuwa inafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wananchi na kutatua
kero zao,”amesema Sumaye
Aidha, Sumaye amewaasa watendaji
wa Serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha
fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni zinafanya kazi
iliyokusudiwa.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kama Serikali
itatumia vizuri rasilimali zilizopo nchini, basi wananchi watanufaika na
kuondokana na umasikini uliokisili na kuleta manufaa kwa Watanzania wote hasa
wale wasiofikiwa na huduma za kijamii.
Post A Comment: