Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Hamis Kigwangalla ametoa sababu za
kutotaja hadharani orodha ya majina ya watu wanaojihusisha kufanya mapenzi ya
jinsia moja.
Amesema hakuweza kuyataja
hadharani majina hayo kwa kuwa alisikiliza ushauri aliopewa na jamii
inayomzunguka.
“Mimi nashaurika, sikuweka majina
hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua
kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo
cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla.
Ameyasema, hayo wakati wa
maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini
Dar es Salaam, amesema kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia
na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.
Aidha, amesema katika sheria
iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna
kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mitindo
isiyoeleweka na ikabainika kuwa ana muonekano wa watu wa aina hiyo, atafunguliwa
mashtaka mara moja.
Hata hivyo, Kigwangalla amewaonya
wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba Serikali
itawachukulia hatua kimya kimya.
Post A Comment: