WATU watatu raia wa Nchi ya Burundi waliopewa hifadhi katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Mkoa wa Kigoma,wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la hapo,kwa tuhuma za upangaji wa magogo katika barabara kuu ya Kigoma ,Kasulu na Kakonko kwa lengo la utekaji wa magari hasa mabasi ya abiria yaendayo mikoani.
Pia, walipokaguliwa walikutwa na vitu vifuatavyo Bomu moja la kutupwa kwa mkono(Offensive hand Grenade),Bunduki moja ya bandia,panga mbili,rungu 3,viatu aina ya raba jozi moja,viatu vya kike jozi moja,simu aina ya nokia Nne,Tecno tatu,vipodozi vya kike,laptop ,power benki,saa,sanjari na nguo mbalimbali za kiume.
Akizungumzia tukio hilo leo mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake kigoma Ujiji,Kamanda wa Polisi Ferdinand Mtui alisema walibaini hilo baada ya askari polisi waliokuwa katik
a doria kwenye njia hiyo yenye mapori makubwa ndipo waliwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwakwenye mtego.Aliyataja majina ya watuhumiwa hao ni pamoja na Hakizimana David(21),Nepomseni Niogere(25) na Nduwamahoro Justine(20) wote ni wakimbizi wanaoishi katika kambi ya mtendeli iliyopo wilaya ya Kakonkona watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Alitoa mwito kwa raia wote wa kigeni waliopewa hifadhi katika kambi mbalimbali za wakimbizi mkoani humo watii sheria,kanuni na taratibuzote za nchi na waache kujihusisha na vitendo
Post A Comment: