Uongozi wa klabu ya Arsenal umekanusha taarifa za kumuwania
meneja wa klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini
Ujerumani, Thomas Tuchel.
Juzi, klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, iliripotiwa
kuwa katika mipango ya kumrithisha mikoba ya Arsene Wenger meneja huyo, ambaye
ameonyesha kuwa na umakini kubwa katika ukufunzi wake tangu alipokubali kupokea
kijiti kutoka kwa Jurgen Klopp.
Arsenal wamekanusha kumfuatilia Tuchel, lakini bado
wanaendelea kushikwa na kigugumizi kuhusu meneja wa mabingwa wa soka nchini
Italia, Juventus aitwae Max Allegri ambaye kwa kipindi kirefu amekua akitajwa
huenda akamrithi Arsene Wenger.
Kutokana na hatua hiyo, bado inaaminika kuwa Allegri huenda
akawa chaguo la kwanza la viongozi wa Arsenal, endapo wataafiki kuachana na
Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wake wa kukinoa kikosi cha
The Gunners utakua unafikia kikomo.
Post A Comment: