Rais Donald Trump amehutubia wabunge wa Marekani muda mfupi uliopita ambapo ameahidi kufufua nguvu na bidii ya Wamarekani.
Amesema kwa muda mrefu, Wamarekani wa kipato cha kati wamekuwa wakipungua na miundo mbinu imedorora, huku maovu kama vile Uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya kupitia mipaka ya Marekani yakiendelea kushamiri.
Bwana Trump amesema ataiomba bunge kuidhinisha bajeti ya dola trilioni moja kwa lengo la kuwekeza katika miundo mbinu ya taifa hilo.
Ameahidi kupunguza kodi inayotozwa kampuni za Marekani, na pia kupunguza kodi kwa Wamarekani wa kipato cha kati.
Aidha Aidha rais Trump amesema kwamba atabadilisha mfumo wa uhamiaji ulioko sasa ambapo watu walio na ujuzi wa chini wanaruhusiwa kuingia Marekani, na kusema kwamba wahamiaji wanaoonekana kwamba wana ujuzi wa hali ya juu na wanastahili kuingia Marekani, wataruhusiwa.
Anasema kazi yake si kulinda ulimwengu, bali ni kulinda Marekani.
Amsema ataunga mkono muungano wa mataifa yanayojihami ya NATO.
Amesisitiza kwamba Marekani itafanya kazi na washirika wake kuangamiza kundi la kigaidi la Islamic state.
Wakati wabunge wa Republican wakishangilia na kufurahia hotuba hiyo, wabunge wa democrat waliketi kimya bungeni, na baada ya hotuba kukamilika, mmoja wao akasema hotuba ya Trump haikuwa ya kuunganisha.
Post A Comment: