Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wawili wakiwa na vipande sita vya meno ya Tembo katika
maeneo ya Chanika Zingiwa nje kidogo ya jijini la Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
salaam, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,
amesema kuwa watuhumiwa hao wa meno ya Tembo walikamatwa wakiwa
wameyaficha katika begi dogo lililokuwa limefichwa kwenye nyasi.
“Watuhumiwa tuliowakanmata ni Senei Abbas mfanyabiashara na mkazi wa
Buguruni na mwingine ni Juma Kong’wa fundi ujenzi mkazi wa Gongo la
Mboto, kila siku tumekuwa tukiwaasa wananchi kuacha kujishughulisha
uhalifu lakini wanaona kama tunatania, sisi popo0te walipo wahari
tutkula nao sahani moja,”amesema Sirro.
Post A Comment: