Wananchi mkoa wa Pwani wamehimizwa kushirikiana katika masuala ya
kijamii ikiwemo suala la usalama na kilimo cha matunda na zao la korosho
na kuondokana na masuala ya migogoro ya wafugaji na wakulima ambayo
imekuwa ikigharimu maisha ya watu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alipokuwa
akihitimisha ziara yake wilayani Kibaha, amesema kuwa mkoa wa Pwani una
viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo endapo
wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.
“Niwasihi wakulima wa mkoa wa Pwani na mikoa jirani kulima kwa bidii
kilimo cha maembe , nyanya, mananasi ,peasi na pilipili na si tu kilimo
tulichokizoea, kwasasa inabidi tubadilike kulingana na wakati kwani
viwanda vinazidi kuongezeka,”amesema Ndikilo.
Hata hivyo katika hatua nyingine, Mhandisi Ndikilo amewaomba
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kukimbilia kuwekeza mkoani Pwani
kwani mkoa huo unaelekea kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji.
Post A Comment: