Hali ya wasiwasi imeendelea
kutanda kutokana na majibizano makali na vitisho kati ya Marekani na
Korea Kaskazini, ambapo meli ya jeshi la Marekani (USS Michigan)
imewasili katika Korea Kusini huku hofu ikiongezeka zaidi kuhusu
uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au
silaha za nyuklia.
Meli hiyo yenye uwezo wa kushambulia kwa makombora, imewasili
kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo
ambapo zinaongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson.
USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyingine ndogo.
Post A Comment: