Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya
Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa
Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo, Awa Dabo.
Aidha, Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na Mkurugenzi huyo
kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na
Menejimenti ya Shirika hilo.
Maamuzi hayo yamefikiwa ili kunusuru kuzorotesha utendaji kazi wa
shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania
endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje imetoa rai kwa UNDP kuwakumbusha
Watumishi kipaumbele chao ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia
malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa
Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo
yamefafanuliwa katika Agenda ya Mwaka 2030.
Post A Comment: