Prof. Maghembe Apiga Marufuku Kusafirisha Mkaa Kutoka Wilaya Moja Kwenda Nyingine Kuanzia Mwezi Julai. Seebait.com 2017

Share it:
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametangaza mabadiliko makubwa katika biashara ya mkaa nchini na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mkaa wowote utakaosafirishwa kutoka wilaya moja kwenda nyingine ili kunusuru misitu inayoteketea kwa kasi hapa nchini.

Amesema hayo jana  wakati akifungua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka kwenye Idara, Vitengo na Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: