Katika kuhakikisha mafanikio ya ukusanyaji kodi yanafanyika kwa
uhakika na kuongeza pato la Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa
fedha 2016/2017.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere
wakati wa mahojiano na Televisheni ya Taifa (TBC) katika kipindi cha
Tunatekeleza.
Amesema, kuwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya
Trilioni 15.105 hadi kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa kukusanya
Shilingi Trilioni 10.87.
Aidha, ameongeza kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha
inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia
Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine
mbalimbali ili kurahisisha watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka
usumbufu,” amesema Kichere.
Hata hivyo, Kichere ameongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato
yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna
baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.
Post A Comment: