Sekta ya madini nchini imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi
na shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia uwekezaji, ikiwemo ujenzi
wa miundombinu muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Aidha, Mchango wa makampuni umekuwa na tija kwa taifa kwa kutengeneza
ajira pamoja na kulipa kodi zinazostahili kulipwa, kuchangia soko la
fedha za kigeni, manunuzi ya huduma pamoja na michango ya hiyari kwa
shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii zinazozunguka makampuni hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa sekta rasmi ya uchimbaji madini
ilitoa ajira 7,355 ambazo ni za moja kwa moja na zaidi ya ajira 3,000
kupitia makampuni ya wakandarasi.
Kwa upande wa kulipa kodi, taarifa hiyo inaonyesha kuwa kati ya mwaka
2009 na 2015 makampuni makubwa yamelipa kodi Serikalini zaidi ya
shilingi billioni 870 ikiwa ni mrahaba na zaidi ya shilingi billioni
680 zililipwa kama kodi ya mapato na kodi nyinginezo ambazo sio za moja
kwa moja.
Hata hivyo, Uendeshaji wa sekta ya madini nchini upo chini ya
Serikali na taasisi zake ambazo ni Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)
na Shirika la Uchimbaji wa Madini la Taifa (STAMICO), ambapo sera
zilizowekwa mwishoni mwa miaka ya 1990 ziliwavutia wawekezaji wageni
ambao walianzisha migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu.
Post A Comment: