makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema, ndugu Ben Saanane amepotea kwa zaidi ya miezi
mitano sasa. Hajulikani alipo. Wazazi wake na rafiki zake wamemtafuta na
kutoa malalamiko bila mafanikio. Wamefikisha taarifa kwa jeshi la
polisi na wamepaza sauti bila kuchoka.
Kuna nyakati suala hili
lilionekana la siasa na ndio maana wengine tulikaa pembeni. Lakini sasa
ni miezi 6, hakuna taarifa juu ya suala hili, nimeona nisikae kimya juu ya
hili.
Taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba alishikiliwa na watu wa Idara ya Usalama na amepotezwa. Jeshi la
Polisi wana taarifa za mawasiliano ya mwisho ya Ben Saa nane kwa kutumia
simu yake ya mkononi, ambayo inaonekana simu ilipoteza mawasiliano akiwa
maeneo ya Buguruni siku aliyotekwa tarehe 15/16 Novemba 2016.
Post A Comment: