Waamuzi Ligi Kuu Tanzania Bara Wapewa Onyo

Share it:
Kamati ya waamuzi ya shirikisho la soka nchini TFF, imewataka waamuzi watakaochezesha michezo ya lala salama ya ligi kuu Tanzania bara kuwa makini na usimamizi wa sheria 17 za mchezo wa soka.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Salum Umande Chama amezungumza na Dar24, na kueleza namna walivyojipanga kuhakikisha kila mchezao unachezeshwa kwa kuafuata maadili na sheria 17 za soka.
Chama, amesema waamuzi wanapaswa kuegemea katika uweledi na kuacha mapenzi na timu fulani, jambo ambalo linaweza likaibua vurugu, ama kuisababishia timu nyingine kukosa haki na kushuka daraja.
“Tunataka kila mwamuzi atakaepata nafasi ya kuchezesha michezo ya mwisho ya msimu huu kuwa makini, na hatutomfumbia macho kama ataboronda kwa makusudi ya kuwafurahisha watu wachache.”
Ninakuhakikishia tupo macho na tutamfuatilia kila mtu ambaye tutampa jukumu la kuchezesha michezo iliyosalia, kila mtu kwa sasa anaiangalia ligi kwa kutaka kufahamu nani atashuka daraja na nani atakua bingwa, tunataka kuona bingwa anapatikana kihalali na watakaoshuka daraja washuke kihalali, sio kwa kukandamizwa.”
“Kamati inawaagiza waamuzi wote kuwa makini na kazi zao na kama itashindikana kufuata maadili ya uamuazi, hatutosita kuwafungia na kuwapandisha waamuzi wengine ambao tayari wameshafuzu Cooper Test.” Amesema Chama.
Ligi kuu ya soka Tanzania bara inatarajiwa kumalizika mwezi ujao na klabu za Simba na Young Africans zinaendelea kuwa sehemu ya kuwania ubingwa wa 2016/17, huku Majimaji FC, JKT Ruvu, Mbao FC, Toto Afrricans, Stand Utd, Ruvu Shooting na Ndanda FC zikiwania kutokushuka daraja.
Share it:

SPORTS

Post A Comment: