Mimi
ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu
kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa
nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.
Sasa
huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho
kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na
kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.
Ila
mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila
anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi
mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije
akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia
ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.
Sasa
please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye
huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?
Post A Comment: