Jamaa mmoja alikuwa anaendesha gari
mitaa ya mjini kati na kukutana na bango kubwa (tangazo) lililoandikwa
" Nunua mafuta ya gari
yako na pata uroda (sex) bure". Jamaa kwa kiwewe akakata kulia na kwenda
katika kituo cha mafuta alichoelekezwa. Baada ya kujaza mafuta akamuuliza muhudumu "vipi kuhusu
uroda wa bure?
bila kuchelewa muhudumu huyo (mwanaume) akampa lundo la tiketi
na kumtaka achague moja . Jamaa akachagua namba 3 na kumpa muhudumu. Muhudumu akaiangalia na kumwambia 'umekosa, jaribu siku
nyingine". Kwa
muda wa mwezi mzima jamaa akawa anapitia katika kituo hicho cha mafuta na
kujaribu bahati yake; hata hivyo hakupata kitu.
Mwisho jamaa akakasirika na kumwambia muhudumu, "nyie matapeli sana, mwezi huu kila siku nimekuwa nikija
kujaza petrol katika kituo hiki, lakini sijafanikiwa kupata uroda wa
bure…inaelekea nyie ni wasanii tu"
Mhudumu akamwambia "sie sio
wasanii, inategemea na bahati ya mtu, kama huamini nenda kamuulize mkeo maana yeye mwezi huu tu ameshashinda mara Kumi na mbili !!
Post A Comment: