SERIKALI
imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya
mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha
wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.
Waziri
Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la Idd
lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro lkitanguliwa na
Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha.
“Kinachofanyika
sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka kuingiza watu
wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya yanafanywa labda na
waislamu hapana .”alisema Mh Majaliwa .
Alisema
kaz kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anashiriki katika
mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza kutoa
ushirikiano kwa kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.
“Kazi
yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tunauthibitisho wa ushiriki wao na hatua kali
zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.
Mapema
katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa na kaimu
katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa na matukio ya
mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani.
Alisema
kutokana na matukio hayo Baraza kuu linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu
na jamaa zao katika matukio hayo aliyoyataja kutokuwa na hata chembe ya
kibinadamu .
“Kumekuwepo
na matukio ya kutisha ya mauaji ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa
Pwani,matukio ambayo yametushtua sana na kuisikitisha mioyo yetu,baraza kuu la
waislamu la Tanzania kwanza kabisa linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu
na jamaa zao katika matukio hayo ya kinyama yasio na chembe ya kibinadamu hata
kidogo.”alisema Abeid
Alisema
Bakwata inasikitishwa na vitendo vyenye viashiria vya kutaka kuichafua dhima
nzuri ya Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu hasa pale matukio hayo
yanapo husishwa na na Dini ya Kiislamu.
“Uislamu
ni dini ya amani upendo kuvumilia na nakuishi pamoja na watu wa imani tofauti
na kwamba yeyote afanyae matendo yoyote na kinyama kama hayo katu haiwakilishi
uislamu na baraza linawataka waislamu kushikamana.”alisema Abeid.
Post A Comment: