HABARI
za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani
zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku hii.Mada leo inahusu
siku za hatari ambazo mwanamke akifanya
ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.
Nimeamua
kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na
kutupa watoto na hata kuwa na watoto wa
mitaani yanasababishwa zaidi na mimba
ambazo hazikutarajiwa.
Mimba
nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga
asipate.
Ni
muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko
katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma,
mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake
wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo
nitawaongelea zaidi.
Ili
kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya
kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi
unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa
mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba
ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama
atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua
mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya
ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina
uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi
48
baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka
tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa
Post A Comment: