“Nasikia uliwekwa ndani kwa ajili ya rambirambi za watoto wa Lucky Vicent,sasa nakupa hizi kawakabidhi wa×wa,
wakikukamata tena nipigie simu.”
Hiyo ilikuwa ni kauli ya mwisho aliyoitoa Mzee Philemon Ndesamburo wakati walipokuwa akisaini hundi kwa
ajili ya kutoa mchango wake wa rambirambi kwa wa×wa wa ajali ya basi Lucky Vicent jijini Arusha.
Ndesamburo alitoa kauli hiyo akiwa o×sini kwake na Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro aliyemuita ili
kumkabidhi rambirambi za watoto 32 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu
Wilayani Karatu.
Akiwa anasaini hundi hiyo, Ndesamburo aliishiwa nguvu, ndipo wakamchukua kumuwahisha Hospitali ya Rufaa
KCMC, Moshi na muda mfupi baada alifariki dunia.
Meya wa Arusha alisema kuwa Ndesamburo alikuwa amepanga kutoa Tsh 100,000 kwa kila familia ya mtoto
aliyefariki.
Philemon Kiwelu Ndesamburo alizaliwa Februari 19, 1935 na kufariki dunia Mei 31, 2017. Alikuwa ni Mbunge
Mstaafu wa Moshi Mjini (2000-2015), na pia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro.
Post A Comment: