Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji
mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi
mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo
yafuatayo yakafuatia:
Mkulima: Baba yako yupo?
Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.
Mkulima: Mama yako?
Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.
Mkulima: Kaka yako Howard yupo?
Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na
mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie
maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa
kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa
mimba binti yangu.
Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema:
Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha
shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng'ombe na elfu hamsini kwa beberu.
Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.
Post A Comment: