ASKOFU
mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa,
Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa
kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.
Akizungumza
baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika
ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema
Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli
na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama
lengo lilivyokuwa.
Askofu
huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na
jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa
kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika
ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada
zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha
rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na
kwa
kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Kweli
nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais
na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.
Hata
hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika
ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo
vya ufundi.
“Katika
kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate
haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto
wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.
Chanzo:
Mtanzani
Post A Comment: