Mkutano wa Sita wa Bunge la 11 uliomalizika Ijumaa iliyopita mjini Dodoma, umeandika historia nyingine kutokana na kuwepo kwa mambo makuu matano yaliyolipa Bunge hilo tofauti na mikutano mingine iliyopita.
Aidha, kwa pamoja wabunge wote bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa walisimamia walichokiamini hivyo kukipa chombo hicho hadhi yake.
Mambo hayo ni pamoja na kupinga wakuu wa mikoa na wilaya kuingilia haki na madaraka ya Bunge, wabunge kukamatwa bila utaratibu, kasoro katika kutaja watu wanaotakiwa kuhojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, kuhoji utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na kusuasua kwa utekelezaji wa sera ya Tanzania kuhusu viwanda.
Hata hivyo, hatua hiyo imelifanya bunge hilo la 11 kuwa tofauti na mikutano iliyopita, mkutano huo ulishuhudia wabunge wakiungana katika hoja hizo bila kujali itikadi zao, jambo ambalo liliwaweka katika wakati mgumu baadhi ya mawaziri huku Spika, Job Ndugai akihitimisha kwa kuonya wateule wa Rais wanaojisahau kwa kutoa lugha zisizoeleweka.
Post A Comment: