Kumekuwepo na taarifa mpaka za video
Watanzania mbalimbali wakiongea baada ya kuondolewa kwa lazima nchini
Msumbiji na kurudishwa Tanzania kwa Malori huku wengine wakisema Polisi
wa Msumbiji wamewanyang’anya simu na pesa walizokua nazo.
Leo Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia Naibu waziri wake imetoa ufafanuzi kuhusu ishu hii kwa kusema
“Mnajua
kabisa uhusiano wa Tanzania na Msumbiji sio mbaya na hata December 2016
tulifanya mkutano na kutazamia maswala ya uhusiano na biashara
“Baada
ya kusikia taarifa za kukamatwa na kuondolewa kwa Watanzania, tulituma
ubalozi wetu kujua ni kitu gani kinaendelea na wameambiwa Serikali ya
nchi hiyo inawaondoa walioingia kwenye taifa hilo isivyo halali“
“Ubalozi wetu kwa Msumbiji wako
pale wanashirikiana na serikali ya Msumbiji, uongozi wa Mtwara na
UHAMIAJI Mtwara pia wako pale wanashughulikia… tunachokifanya sasa hivi
ni kuhakikisha kama ni kweli yale yaliyosemwa na Watanzania ikiwemo
kunyang’anywa hati za kusafiria“
“Tumeambiwa
zoezi hilo la Msumbiji sio tu kwa raia wa Tanzania bali raia wa nchi
mbalimbali walioingia nchini humo bila vibali au kufata taratibu za
kuishi na kufanya kazi nchini humo“
Naibu Waziri ameahidi kutoa taarifa kamili baadae lakini ya kufahamu kwa sasa ndio hayo
Post A Comment: