Kuna matatizo mengine unayoweza kukutana nayo katika simu janja yako yakakulazimisha hadi
uformat simu lakini kumbe kuna kanjia kadogo tuu ungetumia na ungetatua tatizo lako kabisa.
Tatizo la error 505 katika app ya Google Play Store.
Leo fahamu jinsi ya kutatua tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store huku ikukupa neno ‘Error 505’.
Ya kwanza: Zima, washa pia hakikisha muda wa saa
Zima na kuwasha simu yako. Muda mwingine kufanya hili tuu kunaweza ondoa tatizo hili na utaweza kupakua apps bila shida tena. Na pia hakikisha kama saa ya
simu yako inaonesha muda ulio sahihi.
Jaribu kupakua app yeyote tena kupitia Google Play Store, ikikupa error ile ile tena nenda jaribu njia ya pili.
Njia Ya pili: Cache na Data za Google Play Store
Futa Cache na Data za Google Play Store
Nenda Settings
Bofya Apps au kwenye simu nyingine huwa panaitwa Application Manager
Bofya ‘All’ katika eneo la juu
Tafuta Google Play Store katika orodha na kisha ibofye
Hapa utaona machaguo mawili ‘Clear Cache’ na ‘Clear Data’, Bofya Clear Data kisha Clear Cache
Njia ya tatu: Akaunti ya Google
Katika eneo la Accounts bofya Google
Bofya kwenye akaunti yako ya Google na kisha bofya ‘Remove Account’
Zima simu yako na waishe tena
Fuata hatua za kuweka akaunti ya Google upya
Kama njia zote hizo zimeshindikana basi hapa ndio itabidi ufunye maamuzi mazito. Ureset simu yako, kuhusu hili soma – Jinsi ya kureset au kuformat simu ya
Android.
Post A Comment: