WAKUVANGA AGEUKIA MASUALA YA KILIMO

Share it:
Ni muda mrefu sasa tangu wasanii wachekeshaji wa kundi la Original Comedy kusimamisha kuendesha kipindi chao cha Original Comedy,  Sababu maalumu za kusimama kwa kipindi hiko hazijaweza kufahamika mara moja, zaidi ni kile kinachoonekana kufanywa na  wasanii hao kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali tofauti na ile ya uchekeshaji.

Issaya Mwakilasa anayefahamika kwa jina la ‘Wakuvanga’ ameamua kujikita kwenye kilimo kwa sasa ambapo ameweza kufungua kampuni yake inayohusu mambo ya kilimo inayoitwa kilimo Burudani.

Akizungumza Dar es salaam jana, Wakuvanga alisema siku hizi muda mwingi anautumia kwenye kilimo ambapo ana mashamba na amelima mazao mbalimbali huko Bagamaoyo yakiwemo mahindi, mpunga, maharage, mapapai, vitunguu, na mazao mengine.

”Ni muda sasa nimejikita kwenye shughuli za kilimo na nimeanza kupata matunda na mafanikio makububwa ambapo sikutarajia kwakweli, kilimo kinaingizia fedha na watu wengine wanadharau kilimo lakini wajaribu waone matunda yake” amesema Wakuvanga.

Hata hivyo amesema kwa sasa ameanzisha kampuni ya kilimo ambayo yeye ni mwenyekiti na anawakaribisha watu kujiunga katika kampuni hiyo ambapo wataona mafanikio yake.

”Ni kampuni ambayo imekuja kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo Tanzania kwa kuanzia tunaanza na watu 100 ambao watapata huduma ya shamba trekta na umwagiliaji kuanzia wakati wa kupanda hadi mavuno.” amesema Wakuvanga.

Amewashauri watanzania kujiunga na kilimo ili kurahisisha maisha, kwani kilimo kitakuwa burudani kwao  na kuona mafanikio kipindi cha mavuno.
Share it:

ENTERTAINMENT

Post A Comment: