DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA KAMATI YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU NA SHEREHE ZA KUMUAGA ASKOFU NKOLA

Share it:

Jumamosi Februari 18,2017,kumefanyika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mamia ya wachungaji,viongozi na waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro.Mnenaji mkuu katika kikao hicho alikuwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Askofu Dkt. Makala aliwapongeza viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa kanisa hilo,Mchungaji Jakobo Mapambano kwa kuandaa sherehe ya kumuaga Askofu Nkola ambaye amekuwa askofu wa Kanisa hilo tangu tarehe 24.10.1993.

Askofu Makala alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa kanisa hilo kutokuwa na tamaa ya madaraka ya uongozi kwa nafasi itakayoachwa na Askofu Nkola hili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza na kusisitiza kuwa ni vyema kiongozi atakayeziba nafasi hiyo apatikane kwa utaratibu unaotakiwa.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: