ANNE MAKINDA AONGOZA MKUTANO MKUU WADAU BIMA YA AFYA MKOANI SIMIYU.

Share it:


Katika Mkoa wa Simiyu kumefanyika Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfumo wa Bima ya afya nchini (NHIF), Mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Nchini Anne Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka.

Akongea wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, alionekana kukerwa na uwepo wa baadhi ya watoa huduma kutoka katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali nchini kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi juu ya mfuko huo.Mbali na hilo Mwenyekiti huyo alikerwa kwa baadhi ya watoa huduma wa serikali pamoja na watu binafsi, kukidhiri kwa udanganyifu wa madai kwenda NHIF, ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakipeleka madai hewa katika mfuko huo kwa ajili ya kulipwa.

" hii ni changamoto kubwa sana kwa watoa huduma wetu, wamekuwa wakituletea madai ambayo siyo halisi, na kuashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi yao, jambo hili limekuwa kero kubwa sana mfuko na, hivyo ni lazima wachukuliwe katua kuanzia ngazi za halmshauri na mikoa" 

AlisemaMkutano huo umeshirikisha wadau wengi wakiwemo viongozi wa kisiasa, wabunge, Madiwani, wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wahuduma wa afya, watoa huduma binasfi, viongozi wa dini, walimu, watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali, pamoja na wananchi.

Wakichangia mada mbalimbali wadau wengi wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye sehemu za kutolea huduma, licha ya kuchangia mfuko huo kila mwaka, lucha chafu kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya.

" tumekuwa tukitumia muda wetu na wananchi wanatusikiliza na kutuunga mkono kuchangia mfuko huu, lakini malalamiko yamekuwa mengi sana, ukosefu wa dawa pamoja na lugha chafu, hapo ndipo na sisi tunavunjika moyo na hali ya kuendelea kuchangia maana kila tukienda kuhamasisha tunakumbana na maswali hayo na tunakosa majibu" 

Alisema MakondekoMbali na hilo wadau hao walilalamikia mamlaka ya dawa nchini (Msd) kwa kushindwa kutoa dawa za kutosha kwa vituo mbalimbali vya afya nchini, ambapo baadhi waliiomba serikali kuifuta Msd, na kuunda chombo kipya kutokana na kushindwa kazi, huku halmashauri zikiomba kuruhusiwa kununua dawa moja kwa moja bila ya kupitia msd.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: