Picha 8:Benzi Watengeneza Gari la Kifahari Litakalouzwa Kwa Watu 9 tu Duniani.

Share it:


Kampuni ya Mercedes Benz imetangaza toleo lao jipya ya gari za kifahari aina ya Maybach — ambalo ni gari la kifahari lenye muonekano wa gari linaloweza kuhimili barabara mbovu.
Gari hili linaitwa Mercedes G650 Landaulet, lina nafasi kubwa kuliko tulivyozoea gari nyingi zilivyo na viti vyake vimetengenezwa kukufanya ustarehe zaidi ya unapolala kwenye kitanda chako!

Tazama hapa baadhi ya picha za gari hili:
Landaulet ni gari ya kwanza kutoka kampuni ya Maybach kutengenezwa na Benz. Gari hii ilitengenezwa na kuwekwa kwenye kundi la ‘S –Class’, katika jitihada za Benz kuinusuru kampuni ya Maybach.


Gari hii ambayo baada ya kuboreshwa ikaitwa S600 lina vioo visivyoruhusu risasi kupenya na jenereta linalotoa moshi nje ya gari endapo mtakuwa kwenye hatari
Mercedes wakatengeneza gari hili toleo la  S650 Cabriolet ambayo ilikuwa mara ya pili kwao kuboresha gari la kampuni ya Maybach.


Lina viti vine na paa linalofunguka (comvertible)
Gari hili toleo la sasa lina nafasi ya kutosha mtu kukaa na kujiachia. Kuna nafasi ya futi 2 kati ya miguu ya mtu aliyekaa na kiti kingine!


Wanaokaa mbele wanakuwa kwenye paa lililofunikwa wakati wale wa viti vya nyuma wanakuwa kwenye paa linaloweza kufunguka.


Ni kawaida kuwekewa starehe kenye magari aina hii. Kila abiria aliyekaa viti vya nyuma amewekewa televisheni yenye ukubwa wa inchi 10


Limetengenezwa kukupa utulivu wa hali ya juu kabisa uwapo ndani gari. Viti vyake vinaweza kukanda mwili wako (massage) kwa kubonyeza kitufe tu.



Pia kunakioo kinachotenganisha watu walio kwenye viti vya mbele na wale waliokaa viti vya nyuma.


Benz hawajatangaza bado gari hili litauzwa kwa gharama gani lakini endapo itakuwa kama gari nyengine mbili za kampuni ya Maybach ambazo walishazitengeneza awali, lazima litauzwa zaidi ya dola laki tatu za Marekani. Itatengeneza magari 99 tu na kuuzwa kwa mwaka huu.


Ingawa ndani lina muonekano wa gari la starehe, gari hili limetengenezwa kumudu barabara mbovu. Limeinuliwa juu kwa futi 1.7 kutoka ardhini na lina injini yenye nguvu aina ya V12 Biturbo.
Share it:

ENTERTAINMENT

Technology

Post A Comment: