MKURUGENZI MANISPAA YA KINONDONI ATAKIWA KUPELEKA MAMENEJA NA MASHINE ZA KIELEKTRONIC (EFD) KWENYE MASOKO.

Share it:





Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ali Hapi amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anapeleka Mameneja pamoja na mashine za kielektronic(EFD),kwenye masoko kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea.

Ametoa agizo hilo jana alipokuwa akisomewa taarifa ya mapato na matumizi ya Masoko na Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama Bi. Elizabeth Minga ambapo ilionesha upotevu mkubwa wa fedha kwenye masoko hasa soko la wamachinga lililoko Mwenge.Amesema fedha nyingi zinapotea kutokana na kutokuwepo utaratibu mzuri wa kukusanya mapato kwenye masoko.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku uanzishwaji wa vikundi vya kiholela vya kusimamia masoko ili kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea.Kijitonyama ni Kata ya nne kati ya Kata kumi za awamu ya pili zinazotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: