Magwiji wa soka kutoka nchini Argentina Diego Armando Maradona na Lionel Messi watakua sehemu ya wachezaji watakaocheza mchezo wa hisani, utakaoashiria kupinga vitendo vya kigaidi Mei 21 mjini Abuja nchini Nigeria.
Shirikisho la soka duniani FIFA pamoja na lile la Nigeria (NFF) wamekubaliana kuandaa mchezo huo maalum, ambao utaongeza umakini wa ulinzi na usalama kwa wanaadamu popote pale duniani, ambao wapo katika hatari ya kufanyiwa vitendo vya kigaidi.
Wachezaji wengine wanaotarajiwa kushiriki siku hiyo ni Zinedine Zidane, Ruud Gullit, Ronaldinho, George Weah, Samuel Kuffour, Samuel Eto’o, Abedi Pele, Nwankwo Kanu, Austin Jay Jay Okocha, Thierry Henry David Beckham, Didier Drogba na Cristiano Ronaldo.
Wachezaji wa soka upande wa wanawake nao watashiriki kwa ajili ya kuonyesha nguvu yao katika vita hiyo.
Wachezaji hao wa kike ni Sydney Leroux, Asisat Oshoala, Birgit Prinz, Sun Wen, Abby Wanbach, Homare Sawa, Kelly Smith, Marta, Alex Morgan, Hope Solo, Toni Duggan, Anouk Hoogendijk, Nayeli Rangel, Lauren Sesselmann, Julia Simic na Corine Petit.
Post A Comment: