WANASHERIA WAASWA KUWASAIDIA WANYONGE ZAIDI NA KUAACHA KUWASAIDIA WAHALIFU- MAKONDA

Share it:


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam kujitoa kwa kuwasaidia wanyonge na masikini kuweza kupata haki zao na sio kutumia taaluma katika kuwatetea watu wanaofanya uhalifu.

Makonda ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea mrejesho kwa wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa kisheria kwa jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa kuna watu wanakosa haki kutokana na kukosa msaada wa kisheria.

Amesema kuwa wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam wakijitoa watakuwa wamesaidia wananchi kupata haki pamoja na kupunguza migogoro iliyopo.Makonda amesema vijana waliotoa msaada wa kisheria wameonyesha uzalendo na kuwataka kuendelea kuwatumikia wananchi.

Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa Kisheria, Georgia Kamina amesema kuwa wamesaidia makundi mengi ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi.Georgia amesema walichojifunza katika kazi walioifanya ni wananchi kushindwa kujua sheria na jinsi ya kupata haki
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: