MSIMAMO WA NDUGAI UMETUOKOA WABUNGE

Share it:

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa Polisi kuwakamata wabunge hovyo sasa imefikia mwisho baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa uamuzi kuwa Afisa yoyote wa Serikali ambaye atakuwa akimuhitaji mbunge ni lazima kwanza atoe taarifa kwa Spika
Hayo yamefikiwa baada ya Bunge kupitisha azimio la kutaka ruhusa ya Spika wa bunge pale vyombo vya dola kama polisi wanapokuwa wanamhitaji mbunge yoyote kwa jambo lolote.
“Spika wa Bunge ametoa uamuzi wa Spika kwamba Afisa wa Serikali anapomtaka mbunge kwa jambo lolote lile lazima kwanza kupata kibali chake, Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola hulinda kwa wivu mkubwa hadhi yake kama mhimili,”amesema Zitto.
Aidha, mbali na hilo, Zitto Kabwe ametoa pongezi kwa wabunge wote pamoja na Spika wa bunge kwa kuonyesha msimamo na mshikamano wa kupigania heshima ya bunge.
Share it:

EAST AFRICA NEWS

Post A Comment: