Msanii Nikki Mbishi ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'I'm sorry JK', huenda akaingia matatani baada ya kutakiwa kuripoti katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu ujumbe uliomo kwenye wimbo huo.
Katika wimbo huo Nikki anaonesha kumuomba radhi aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete huku akidai kuwa Watanzania hadi sasa tayari wameshamkumbuka Rais huyo mstaafu kutokana na namna alivyokuwa akiongoza nchi, akifananisha na namna ambavyo uongozi mpya umekuwa ukiendesha nchi.
Nikki ndani ya ngoma hiyo kuna mstari anasema "Mikopo hakuna tena na wala chuoni watu hawaendi kizembe", ukiwa ni mstari mmoja kati ya mistari kadhaa ambazo huenda zikawa ndiyo sababu ya BASATA kuhitaji maelezo ya kujirishisha kutoka kwake kiasi cha kumuomba afike ofisini ili kujadili mustakabali wa wimbo huo.
Kwa upande wake Nikki Mbishi amesema amechelewa kupata ujumbe huo wa BASATA kutokana na matatizo ya msiba hivyo alishindwa kufika kwa muda ambao ulikuwa umepangwa ila anasema kwa kuwa aliitwa atafika BASATA na kujadili nao.
"Leo (jana) tarehe 13/02/2017 nimehitajika kuripoti ofisi za BASATA ambapo wanadai walinitumia ujumbe zaidi ya siku 3 nyuma ila sikuwa hewani labda kwa sababu ya msiba ulionipata, kufuatia ujumbe niliyotumiwa juzi tarehe 09/02/2017 kwa njia ya message za kawaida za simu ya kiganjani". Amesema Nikki
"Akiutaja ujumbe huo, Nikki amesema ujumbe ulikuwa unasema "Habari za jioni? Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa " I AM SORRY JK" aliandika Niki Mbishi
Navigation
Post A Comment: