Sababu ya wasichana kutopenda kutaja umri wao

Share it:



Mara nyingi wanawake hasa wasichana wengi hudanganya pindi wanapoulizwa umri wao. Achia mbali kudanganya, wengine wanakasirikia kabisa kiasi kwamba mnaweza hata kugombana tatizo likiwa ni kwanini umuulize umri wake.
Kuna msemo wa zamani uliokuwa ukisema kuwa, Mwanamke hasemi hadharani umri wake halisi, na kwao ni jambo la ajabu na la kukera sana pindi mwanaume anapomuuliza umri wake. Kwa urahisi unaweza kusema kuwa hili kwao ni mwiko.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha wanawake/wasichana kukataa kusema umri wao ni hali ya kuogopa kumkatisha tamaa yule ampendaye. Wanaume wengi hawapendi kuwa kwenye uhusiano na wanawake waliowazidi umri, hivyo wanahofia kama akiwa amemzidi mwanaume umri basi huenda ikawa ndio mwisho wao.
Kuwa na umri mkubwa si jambo baya kwani wahenga husema kuwa busara huja na umri. Lakini kwa wanawake hii ni tofauti, wao wanaamini kuwa ukijitangaza kuwa una umri mkubwa basi kama hujaolewa unaweza usiolewa sababu wanaume wanataka wasichana wadogo wadogo. Unaweza ukamuuliza mwanamke leo una miaka mingapi akakwambia 25, ukirudi baada ya miaka mitatu na kumuuliza akakwambia 25.
Wale wanaosema kuwa umri haujalishi chochote bali ni namba tu, hao wanatafuta kujifurahisha wenyewe baada ya kuona hakuna wanachoweza kufanya tena.
Angalia katika tasnia ya urembo, watangazaji wa runinga na majarida mbalimbali, yote haya yamepambwa na wasichana wenye umri mdogo na muonekano wa kuvutia, hii ndio sababu hawapendi kutaja umri wao ili hata wawe wanadanganya.
Kingine cha kushangaza ni kuwa, wanawake wanapokuwa na umri mdogo zaidi hujikuza na kusema wana umri mkubwa, mfano miaka 15 atakwambia 18 na mwenye miaka 30 atakwambia 24. Wakati mwingine hata waume hawajui umri halisi wa wake zao kutokana na kutopenda kuzungumzia umri.
Ukweli usiopingika, swali “una miaka mingapi” huwakwaza wanawake wengi sana, kuepusha vita usipende kumuuliza msichana hili swali.
Mambo mengi yanayofanyika katika jamii huhitaji wanawake wengi umri mdogo na hivyo wanawake kulazimika kutumia vipodozi vya kila namna ili tu wanaonekane bado ya wasichana wadogo. Msichana atatumia gharama yoyote kuhakikisha anaondoa makunyazi kwenye ngozi yake.
Share it:

HOME

Post A Comment: